Rais wa Sudan Kusini awafuta kazi makamu wa rais na mkuu wa ujasusi

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amewafuta kazi makamu wake wawili, James Wani Igga na Hussein Abdelbagi Akol ikiwa ni mabadiliko ya karibuni kabisa katika serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo.