
Nchini DRC, Mahakama yakijeshi imefunguwa kesi mjini Bukavu dhidi ya askari 84 wa jeshi la Congo wanaotuhumiwa mauwaji ya watu wasiopunguwa 9 wilayani Kabare na uporaji wa mali ya raia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Baadhi ya askari hao ni wa kikosi kinachoitwa Duma au Guépard, wakituhumiwa kwa mauaji, wizi, uporaji, uasi, kumtoroka adui, ubakaji na kadhalika.
Mugoli Alice Civarara ni mkazi wa Cirato katika kijiji cha Kavumu, ameponyokea chupuchupu mauaji nasasa anashiriki kesi hii :
“Mimi nigependa kutendwa haki, watu hao wafungwa kwa sababu hawakuchagua mtoto wala mtu mzima.” Alisema Mugoli Alice Civarara ni mkazi wa Cirato katika kijiji cha Kavumu.
Jumamosi, askari wenye silaha walipora maduka na masoko madogo-madogo pia mjini Bukavu na kufyatua risasi hewani.
Hali hii pia ilishuhudiwa katika kijiji cha Nyangezi Jumapili jioni, wakazi wengi wa vijiji tangu Katana hadi Mumosho wakitoa malalamiko. Justin Mulindangabo ni msimamizi wa asasi za kiraia wilayani Kabare, anataka askari hao waadhibiwe inavyostahili.
“Hawa askari wameonyesha kwamba wanafanya kazi na adui na watu waliopoteza lazima wajue wataishi namna gani tena.” Alieleza Justin Mulindangabomsimamizi wa asasi za kiraia wilayani Kabare
Jeshi la Kongo linasema linasikitishwa na hali hii, na linathibitisha kukamatwa kwa askari hao waliotoka vitani na waliofanya maovu hayo dhidi ya raia. Meja Nestor Mavudisa ni msemaji wa eneo la tatu la ulinzi nchini Kongo, anasisitiza kuwa jeshi la Kongo halitawavumilia askari wasio na nidhamu ambao wanachafua sura ya jeshi hilo .
Awali, Gavana wa Kivu Kusini Profesa Jean-Jacques Purusi ametaka kwamba kesi hiyo ifanyike katika vijiji vile mlimofanyika mauaji ili askari hao wajibu kwa makosa yao mbele ya Mahakama yakijeshi na wahukumiwe wakiwepo raia waathirika.
William Basimike- Bukavu RFI Kiswahili.