Trump: Canada ‘haifai’ kama nchi bila misaada ya Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani ameendelea kutoa kauli za dharau na kejeli dhidi ya nchi mbali mbali duniani, mara hii akiishambulia tena moja ya waitifaki wake, akisema Canada “haifai” kama nchi bila msaada wa kiuchumi na ulinzi wa kijeshi wa Marekani.