Trump atamka rasmi: Marekani itawahamisha Wapalestina na ‘itaitwaa’ na ‘kuimiliki’ Ghaza

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza hadharani kwamba Marekani itachukua udhibiti wa Ukanda wa Ghaza, na kulijenga upya eneo hilo lililoharibiwa na vita na kuandaa fursa za kiuchumi kwa wakazi wake wa baadaye.; na alipoulizwa kama atapeleka huko wanajeshi wa Marekani, Trump ameapa “kufanya kitakacholazimu.”