Mzozo wa DRC: Mawaziri wa ulinzi, wakuu wa majeshi SADC kutua DRC

Mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika umeagiza kutumwa mara moja kwa mawaziri wa ulinzi na wakuu wa ulinzi kwa nchi zinazochangia wanajeshi nchini DRC, ili kuhakikisha wanajeshi wa ujumbe wa SADC katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (SAMIDRC) wako salama