#HABARI: Zaidi ya watu 400 wamepatiwa huduma ya msaada wa Kisheria bure, kwenye ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani Mororogo.
Timu ya Wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria chini ya Kampeni ya Mama Samia Legal Aid, walioambana na Rais Samia, kwenye ziara hiyo walikutana na wananchi ana kwa ana, kuwasikiliza kisha kutoa msaada juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ikiwemo migogoro ya Ndoa, Ardhi, mirathi, matunzo ya Watoto, ukatili wa kijinsia.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria Lusajo Mwakabuku.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.