Familia za wahanga zaishtaki serikali ya Afrika Kusini kwa jinai za ubaguzi wa rangi

Familia 25 za wahanga na manusura wa jinai za kisiasa zilizofanyika zama za ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini zimemfungulia mashtaka Rais wa Cyril Ramaphosa wa nchi iyo na serikali yake kwa kile zinachosema ni kushindwa kuchunguza ipasavyo makosa hayo na kutoa haki mkabala wa jinai hizo za kisiasa.