HAMAS: Israel imeshambulia kwa mabomu mahali alipokuwa anashikiliwa mateka mmoja wa Israel

Abu Ubaydah, msemaji wa Brigedi za Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel jana Alkhamisi lilishambuliwa kwa makusudi eneo ambalo mateka mmoja wa kike wa Israel alikuwa akishikiliwa kwenye Ukanda wa Ghaza.