
MANCHESTER, ENGLAND: Leo itakuwa ni mwendelezo wa michuano ya Europa League ambapo kocha wa Manchester United, Ruben Amorim atakuwa na mtihani mwingine mbele ya FK Bodo/Glimt katika mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Old Trafford kuanzia saa 5:00 usiku.
Huu utakuwa ni mchezo wapili kwa Amorim ambaye alianza vibaya baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ipswich Town katika Ligi Kuu England.
Man United inahitaji matokeo ya ushindi katika mchezo huu ili kupanda katika nafasi nane za juu katika msimamo kwani sasa ilipo nafasi ya 15 ikimaliza hapo itatakiwa kucheza mchezo wa mtoano kufuzu hatua ya 16 bora.
Hii itakuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana katika mechi ya kimashindano na Glimt inaingia ikiwa katika msimu wake bora na ndio vinara wa Ligi Kuu Norway hadi sasa.
Mbali ya mchezo huu, moja kati ya mechi kubwa inayoonekana kuwa itafutailiwa sana ni ile ya Tottenham dhidi ya AS Roma itakayopigwa saa 5:00 usiku,Tottenham Hotspur Stadium.
Tangu kuanza kwa msimu huu Roma imekuwa na wakati mgumu sana na ililazimika kufukuza kocha wao Ivan Juric Novemba 10.
Kwa sasa inashika nafasi ya 20 katika msimamo ikiwa na pointi tano wakati Spurs ikishinda nafasi ya saba kwa pointi zao tisa.
Vinara wa ligi hii, Lazio watakuwa uwanjani kuumana na Ludogorets ambayo itapigwa saa 2:45 usiku ikiwa itashinda mechi hii itafikisha pointi 15 na kuzidi kujiwekaea mizizi katika msimamo wa ligi.
Vilevile Ajax ambayo inashika nafasi yapili itakutana na Real Sociedad iliyopo nafasi ya 25. Tangu kuanza kwa msimu huu Ajax imefanya vizuti katika michuano hii ikiwa mechi tatu kati ya nne na kutoa sare moja.