
Baada Ligi ya Mabingwa Ulaya kutimua vumbi siku ya Jumanne na Jumatano, leo ni zamu ya mashindano ya Europa pamoja na Ligi ya Conference ambapo Chelsea na Manchester United zitakuwa dimbani kupambana dhidi ya wapinzani wao.
Timu nyingine kubwa zitakazocheza ni Tottenham Hotspur, Galatasaray, AS Roma na Fiorentina zitakapokuwa kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu.
Manchester United inashiriki michuano hii ikiwa imecheza jumla ya mechi tatu, huku ikiwa haijapata ushindi wala kupoteza baada ya kuambulia sare yote.
Mchezo wa kwanza Man United ilicheza Septemba 25, 2024 ambapo ilipata sare ya bao 1-1 dhidi ya FC Twente inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uholanzi, Oktaba 3, 2024 ilicheza na Porto ikiambulia sare ya mabao 3-3 wakati Oktoba 24, 2024 ilicheza na Fenerbahçe ikipata tena sare ya bao 1-1.
United leo itaingia kucheza dhidi ya PAOK kwenye uwanja wa Old Traford huku ikiwa chini ya kocha wa muda Ruud van Nistelrooy anayeiongoza baada ya kuondolewa kwa Eric Ten Hag.
Mchezo mwingine mkali utakuwa kati ya Galatasaray watakao kuwa nyumbani kuikaribisha Tottenham Hotspur, Roma itakuwa ugenini dhidi ya Union Saint-Gilloise, Lazio itakuwa nyumbani na kibarua kigumu dhidi ya Porto wakati Fenerbahçe itakuwa ugenini dhidi ya AZ Alkmaar.
Chelsea itakuwa nyumbani ikiwakaribisha Noah ya Armenia akiwa inaongoza msimamo wa Ligi ya Conference kwa pointi sita baada ya kushinda michezo yote miwili sawa na Fiorentina ya Italia iiyopo nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao.
Ikumbukwe mfumo wa sasa timu 36 zitakuwa zikicheza mechi nane kwenye mfumo wa nyumbani na ugenini.
Timu nane zitafuzu moja kwa moja kwenda hatua ya 16 Bora timu nyingine 24 zitacheza mtoano na nane zitakwenda hatua ya 16 Bora ambazo zitaingia robo fainali na nusu fainali, kabla ya mbili kucheza mchezo wa fainali mwakani.
Idadi ya michezo kwenye mfumo huu mpya imebadilika kutoka michezo 125 kwenye mfumo uliopita na kuwa 189.
Mechi za leo Europa
Union Saint vs Roma
Midtjylland vs Olympiacos
Rangers vs Galatasaray
Tottenham vs Frankfurt
Slavia Praha vs Nice
Twente vs Bodø
Qarabag vs ElfsborgIF
Braga vs Hoffenheim
Lyon vs Lazio
Porto vs AZ Alkmaar
Fenerbahçe vs Dynamo Kyiv
Man United vs PAOK
Ajax vs Tel-Aviv
Viktoria vs Sociedad
Mechi za leo Conference
Reykjavík vs Borac
Legia vs Dinamo Minsk
Pafosvs Astana
HJKHJK vs Olimpija
Shamrock Roversvs New Saints
Gent vs Omonoia
Topola vs Lugano
Petrocub vs Rapid Wien
Vitória vs Mladá
APOEL vs Fiorentina
LASK vs Cercle Brugge
Hearts vs Heidenheim
Chelsea vs Noah
Djurgården vs Panathinaikos
Copenhagen vs İstanbul
Larne vs GallenSt
Real Betis vs CeljeCelje