Tuujue Uislamu (28)

Ni wasaa na wakati mwingine wapenzi wasikilizaji tunapokutana katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Tuujue Uislamu.

Katika kipindi chetu cha juma hili tutaendelea kubainisha baadhi ya sifa zingine za Mwenyezi Mungu. Kuweni nami hadi mwisho wa kipindi hiki, hii ikiwa ni sehemu ya 28 ya mfululizo huu.

 

Kuumba na uumbaji ni miongoni mwa sifa nyingine za Mwenyezi Mungu, ambazo ni miongoni mwa sifa za matendo yake. Hii ina maana kwamba Mungu pekee ndiye muumbaji wa ulimwengu na hakuna muumbaji isipokuwa Yeye. Hata hivyo neno kuumba au kuunda au kukifanya kitu ambacho hakikuweko na kikawa, ni neno ambalo wakati mwingine linatumika kwa wanadamu, kama tunaposema kwamba mchoraji aliunda na kubuni kazi ya sanaa. Kwa maana kwamba, alikileta kitu ambacho awali hakikuweko. Lakini ifahamike kwamba Mungu ndiye anayetoa msingi wa lazima wa uvumbuzi na uumbaji ndani ya mwanadamu. Yaani mwanadamu kwa kutumia kipaji na uwezo aliopewa na Mungu ana uwezo wa kufanya mambo mapya na kuunda kazi mpya, wakati ubunifu wa Mungu ni wake mwenyewe na hautegemei kuwepo kwa sababu nje ya asili ya Mungu.

Aya ya 16 ya Surat Raad inasema: Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!

Kwa mujibu wa aya hii, Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu ambacho kimevikwa uwepo. Yeye pekee ndiye muumba wa viumbe na amevipa uwepo.

Jambo lingine ni kwamba viumbe wa ulimwengu siku zote na daima ni wahitaji wa Mungu, na hakuna kiumbe kisochomuhitajia Mwenyezi Mungu kwa ya hali yoyote. Kwa mfano mwanadamu, ambaye anamhitaji Mungu kwa ajili ya kutokeza kwake, hatawahi kuwa bila Mungu baada ya kuwa na kuingia katika mandhari ya uwepo.

 Haja ya mwanadamu kwa Mungu haikomei tu katika kudhamini chakula, mavazi na mahitaji mengine ya maisha, lakini anamhitaji Mungu kwa kila kitu ambacho uwepo wa mwanadamu unategemea hilo.

Kwa sababu mali na suhula zote za kimaada na kimaanawi kama vile uhai, afya, usalama, uwezo wa kufikiri, ujuzi na nguvu vinatolewa na Mwenyezi Mungu kwa sura ya kuendelea na kulingana na mapenzi yake. Hivyo mwanadamu anamhitaji Mungu ambaye ndiye muumbaji wake katika nyanja zote za uwepo wake.

 

Kuhusu uumbaji wa Mungu, ni muhimu kutaja kwamba Mungu ndiye muumbaji wa vitu, na amevipa sifa maalumu na sheria zinazoongoza vitu.

Kwa mfano, Mwenyezi aliumba jua na mwezi na akavipa joto na mwangaza. Bila shaka, wakati wowote anapotaka, anaweza kuvikonya jua na mwezi sifa hizi.

Ingawa sifa ya uumbaji ni ya Mungu pekee, lakini hii haipingani na hiari ya mwanadamu katika matendo yake, kwa sababu nguvu zetu, akili, hisia, na hata hiari yetu yote vinatoka kwake. Mungu ndiye muumbaji (wa kila kitu na hata matendo yetu) na kwa upande mwingine, sisi tuna hiari katika matendo yetu na Mungu hajamtenza nguvu mwanadamu. Yeye ndiye muumbaji wa njia zote za matendo na sisi ni watumiaji wa njia hizi katika njia ya wema au shari.

Kuhusiana na uumbaji wa Mwenyezi Mungu, Qur’an tukufu inasema katika Aya ya 62 ya Surat Ghaafir kwamba:

Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi, Muumba wa kila kitu. Hapana mungu ila Yeye; basi mnageuzwa wapi?

Tunajifunza kutokana na Ayah ii kwamba, Mwenyezi Mungu ni Mola na Mlezi na  ni muumba; na uumbaji ni kitu chenye kuendelea na cha kudumu. Kazi ya Mungu si kuumba viumbe na kukaa kando, lakini kila lahadha, neema ya kuwepo inaenea juu ya viumbe vya ulimwengu, na uumbaji wa kila mmoja wao hupokea uwepo kutoka kwa dhati yake safi. Kama inavyosema sehemu ya Aya ya 164 ya Surat al-An’am:

Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu?

Kwa hiyo, uumbaji na mpangilio wa ulimwengu ni kama mwanzo wa uumbaji wa vitu vyote mikononi mwa Mungu. Kwa maneno mengine, ubunifu haujitenganishi na Ubwana, yaani, kupanga na kusimamia ulimwengu wa kuwepo, na kimsingi, kupanga maisha yote kunahusishwa na uumbaji.

Kwa hiyo, uumbaji na mpangilio wa ulimwengu ni kama mwanzo wa uumbaji ambapo vitu vyote viko mikononi mwa Mungu. Kwa maneno mengine ni kuwa, uumbaji haujitenganishi na sifa ya ulezi yaani, kupanga na kusimamia ulimwengu wa uwepo, na kimsingi, kupanga maisha yote kunahusishwa na uumbaji.

Kwa uweza huo, Mwenyezi Mungu ni Muumba wa mbingu na dunia na kila kilichomo ndani yake, naye ni Mlezi wa viumbe vyote na Mpaji riziki kwa kila chenye uhai ulimwenguni.

Hivyo basi kama tulivyotangulia kusema ni kuwa, Muumba ni sifa mojawapo ya Mwenyezi Mungu, kutokana na imani ya kwamba ndiye aliyesababisha vyote vianze na vidumu kuwepo.

Wapenzi wasikilizaji kwa leo tunakopomea hapa. Tukutane tena katika sehemu nyingine ya mfululizo huu.