67 wauawa katika shambulizi la wanamgambo kwenye mji wa El Fasher, magharibi mwa Sudan

Jeshi la Sudan SAF limetangaza kuwa, takriban watu 67 waliuawa Jumapili katika shambulizi la mizinga lililofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini la magharibi mwa Sudan.