Serikali inaendelea kusisitiza umuhimu wa viwanda vidogo vinavyoendana na ukuaji wa teknolojia ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na kuimarisha ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini.
Katika kuunga mkono hilo, Pelina Mgaya, mwanamama mbunifu ameamua kutumia kifaa maalum cha kukaangia karanga kilichobuniwa hapa nchini ambacho kinamsaidia kujipatia kipato chake cha kila siku.
Pelina ni mfano wa wanawake wanaochangamkia fursa za kisasa katika mnyororo wa thamani ya mazao.
#azamnewsupdates
✍Mwanaidi Waziri
Mhariri| @official_jennifersumi