Watu 18 wamefariki dunia kwa mkanyagano uliotokea katika kituo kikuu cha reli jijini New Delhi, India jana usiku.
Tukio hilo limetokea saa mbili usiku jana Februari 15, 2024 wakati maelfu ya abiria, wengi wao wakiwa mahujaji wa Kihindu waliokuwa wakielekea kwenye tamasha la Maha Kumbh huko Prayagraj.
Mkanyagano huo uliripotiwa kuanza baada ya baadhi ya abiria kuteleza na kuanguka kwenye daraja la miguu linalounganisha vituo vya treni, jambo lililosababisha taharuki kubwa.

Miongoni mwa waliopoteza maisha ni wanawake 14 na watoto watano, huku waathiriwa wakiwa na umri kati ya miaka saba na 79.
Watu 12 wamejeruhiwa na wanapatiwa matibabu hospitalini.
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametoa pole kwa familia zilizoathirika.
Waziri wa Reli, Ashwini Vaishnaw ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Wiki chache zilizopita mkanyagano mwingine kwenye tamasha la Maha Kumbh ulitokea na kusababisha vifo vya watu 30.
Endelea kufuatilia Mwananchi.