✍️✍️ na Dr. Angela Nanyaro, Meneja Mwandamizi – Madai ya Matibabu
Afya ya mama ni msingi wa jamii yenye afya. Tunapowatunza wakina mama, tunaziimarisha familia, jamii, na vizazi vijavyo. Kusaidia afya ya mama kunamaanisha kuhakikisha wanawake wanapata huduma bora kabla, wakati, na baada ya kujifungua, yaani, mnyororo wa huduma unaolinda maisha ya mama na mtoto.
Kabla ya kujifungua, upatikanaji wa huduma za kliniki za wajawazito husaidia kugundua na kudhibiti matatizo mapema. Msaada wa lishe, elimu ya afya, na uchunguzi wa mara kwa mara huwapa wajawazito uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yao na watoto wao.
Wakati wa kujifungua, wahudumu wa afya wenye ujuzi, mazingira salama ya kujifungulia, na huduma za dharura kwa wakati ni muhimu ili kupunguza vifo vya mama na mtoto mchanga. Hata hivyo, huduma haipaswi kuishia baada ya kujifungua. Msaada wa baada ya kujifungua, ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya akili, mwongozo wa unyonyeshaji, na huduma za uzazi wa mpango, ni muhimu kwa afya ya mama na maendeleo ya mtoto. Kwa bahati mbaya, wanawake wengi bado hukosa huduma hizi, hasa katika jamii zisizohudumiwa ipasavyo.
Hapa Jubilee Health, tunaamini kwamba kulinda afya ya mama ni msingi wa maisha yaliyojaa furaha na uhuru. Kupitia programu yetu ya Maisha Fiti, tumejitoa kuandamana na kila mama katika safari yake, si kwa kumpatia huduma pekee, bali kwa kujenga jamii hai na yenye mshikamano. Jumuiya ya Maisha Fiti inawaunganisha wanawake na wataalamu wa afya wanaoaminika, inatoa msaada wa kijamii baina ya wanawake, na inawapa maarifa kupitia maudhui ya kielimu yanayoandaliwa na wataalamu.
Kupitia programu yetu maalum ya Mums Club, kina mama hupata nafasi ya kushiriki matukio yaliyopangwa kwa uangalifu ili kuwasaidia, kuwahabarisha, na kusherehekea kila hatua ya uzazi. Kwa kuwekeza katika afya ya mama, tunawekeza katika maisha bora, imara, na yenye matumaini kwa wote.
@jubileeinsurancetanzania