ٌWanajeshi 110 wa Israel wameangamizwa tangu Tel Aviv ianzishe mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya Lebanon

Idara yha Oparesheni ya Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon imetangaza kuwa, hadi sasa wanajeshi 110 wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa na wengine 1,050 kujeruhiwa tangu jeshi la Iutawala huol lilianzishe mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya Lebanon, Oktoba Mosi mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na idara hiyo imesema kuwa: Hadi sasa wanajeshi 18 wa Kizayuni wameangamizwa na 32 kujeruhiwa tangu kuanza kwa awamu ya pili ya mashambulizi ya nchi kavu ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon tarehe 12 Novemba mwaka huu; huku baadhi yao wakiwa katika hali mbaya. 

Wanamuqawama wa Hizbullah ya Lebanon 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tangu Israel ianzishe mashambulizi dhidi ya Lebanon hadi sasa; vifaru 53 vya merkava, magari kadhaa ya deraya, mabuldoza 9 ya jeshi la Israel na zana nyingine za kijeshi vimeangamizwa na wanamuqawama. 

Wakati huo huo, harakati ya Hizbullah imetangaza kuwa imeipiga kwa makombora kambi ya kijeshi la Galilot karibu na Tel Aviv. Kambi hiyo ni makao makuu ya ujasusi ya kitengi cha 8,200 cha jeshi la Israel.